Jumanne, Machi 29, 2016

KUNYONYESHA MTOTO KUTAMUEPUSHIA MAGONJWA YA DAMU

Utafiti mpya uliofanywa Marekani umeonesha kuwa, kuwanyonyesha watoto wachanga kunaweza kuwapunguzia hatari ya kupata ugonjwa wa damu. Watafiti wanaona kuwa, vitu vya kingamaradhi vilivyomo kwenye maziwa ya mama vinaweza kusaidia ukuaji wa mfumo wa kinga wa watoto wachanga.
Ugonjwa wa damu ni saratani inayoonekana zaidi ya watoto, ambayo kiwango ni asilimia 30. Watafiti wa chuo kikuu cha Haifa cha Israel wamewatafiti watoto elfu 10 wanaopata ugonjwa wa damu na watoto wengine elfu 18 wa kawaida.
Matokeo yameonesha kuwa kwa kulinganishwa na watoto wasionyonyeshwa na maziwa ya mama, hatari ya ugonjwa wa damu ya watoto walionyonyeshwa inapungua kwa asilimia 11.
Watafiti wameshauri kuwa maziwa ya mama yanapatikana kwa urahisi, ambayo yana faida nyingi za kiafya kwa watoto wachanga. Hivyo kuwanyonyesha watoto kunatakiwa kutangazwa zaidi kwa kina mama na jamii nzima.

0 comments:

Chapisha Maoni