Utafiti mpya umeonesha kuwa kula kokwa kadhaa kila siku kunasaidia kupunguza hatari ya kufariki mapema inayosababishwa na maradhi ya saratani na ugonjwa wa kisukari.
Watafiti wa chuo kikuu cha Maastricht cha Uholanzi wamefanya utafiti wa kulinganisha uliodumu miaka 10. Walichunguza takwimu za mtindo wa maisha na chakula cha kila siku cha watu zaidi ya laki 1.2 wa Uholanzi. Takwimu hizo zilikusanywa mwaka 1986, wakati ule umri wa watu hao ni kati ya miaka 55 hadi 69.
Baada ya miaka 10, watafiti walichambua kiwango cha kifo cha watu laki 1.2. Wakagundua kuwa kwa kulinganishwa na watu wasiokula kokwa, kiwango cha kufariki mapema cha watu wanaokula kokwa au karanga zaidi ya gramu 10 kwa siku kinapungua kwa asilimia 23.
Lakini watafiti wamesema, matokeo ya utafiti huo hayamaanishi kuwa vyakula vyote vya kokwa na karanga vitaleta faida kwa afya, kwa mfano siagi ya karanga haifai afya kutokana na chumvi nyingi na mafuta mengi.
0 comments:
Chapisha Maoni