Jumanne, Machi 29, 2016

KAMATI YA BUNGE YA SHERIA KUSIKILIZA MAONI YA WADAU, HAPA ZIPO NJIA ZA KUTUMA MAONI YAKO

Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) kwa mujibu wa Kanuni ya 117 (9) kuhusiana na Sheria Ndogo zilizowasilishwa na Serikali katika Mkutano wa Pili wa Bunge uliomalizika Februari 2016.
Mikutano hiyo ya kusikiliza maoni ya wadau kuhusu Sheria Ndogo inatarajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 4 Aprili, 2016 na Jumanne tarehe 5 Aprili, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Sheria Ndogo ambazo Kamati inakaribisha wadau na umma kwa ujumla kutoa maoni yao ni pamoja na zifuatazo:-
The Petroleum (Bulk Procurement) Regulations, 2015
The Public Private Partnership Regulations, 2015
The Copyright and Neighboring Rights (Copyrighted Works – Communication to the Public) Regulations, 2015
The National Examinations Regulations, 2015
The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ General Welfare, Conduct and Disciplinary Matters) Regulations, 2015
The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ Performance Assessment) Regulations, 2015
The Fire and Rescue Force (Fire Precautions in Buildings) Regulations, 2015
Sheria Ndogo zilizotajwa hapo juu pamoja na nyingine ambazo zinashughulikiwa na Kamati, zinapatikana kwa kupakua (downloadable) katika tovuti ya Bunge la Tanzania ya www.parliament.go.tz pamoja na tovuti ya Serikali ya www.tanzania.go.tz
Aidha, maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya posta au barua pepe kwa anuani ifuatayo:-
Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge,
L. P. 9133, DAR ES SALAAM
Barua pepe: cna@bunge.go.tz

0 comments:

Chapisha Maoni