Jumamosi, Machi 19, 2016

JIPU LA NEYMAR LATUMBULIWA!!! BAADA YA KUKWEPA KODI SASA KUILIPA SERIKALI YA BRAZIL BILIONI 110

http://static.goal.com/2667900/2667912_heroa.jpg
Mahakama moja ya Brazil imeagiza mchezaji nyota wa Barcelona, Neymar kulipa reais milioni 188.8 ( Dola milioni 53 za Kimarekani sawa na bilioni 110 za kitanzania) katika kodi, riba na faini baada ya kumpata na hatia ya ukwepaji kodi
Jaji katika mahakama ya shirikisho huko Rio de Janeiro alitoa uamuzi kuwa Neymar alishindwa kutangaza mapato kutoka klabu yake ya sasa Barcelona, klabu yake ya zamani Santos na mdhamini Nike gazeti zilisema kwa taarifa.
Mchezaji huyo mweye umri wa miaka 24 anatarajiwa kukata rufaa. kulingana na utafiti wa jaji Neymar alitumia kampuni kuepuka kulipa milioni 63.6 katika kodi.

0 comments:

Chapisha Maoni