Maini yenye mafuta yanaweza kusababisha maradhi mengi ya ini. Watafiti wa chuo kikuu cha Tsukuba cha Japani hivi karibuni wamegundua kuwa kama watu wanene watafanya mazoezi ya dakika 250 kila wiki, mafuta ya maini yatapungua na kuboresha hali ya maini yenye mafuta.
Watafiti hao waliwatafiti wagonjwa 169 wenye umri wa miaka 30 hadi 69 wa maini yenye mafuta yasiyotokana na ulevi. Ulaji wa kupita kiasi na ukosefu wa mazoezi ni chanzo cha wagonjwa hao kupata maini yenye mafuta.
Kwa mujibu wa muda wa mazoezi waliyoyafanya kila wiki, watafiti waliwagawanya kwa vikundi vya dakika sizizozidi 150, dakika 150 hadi 250 na dakika zinazozidi 250, na kuchunguza kama hali ya maini yenye mafuta itaboreka au la baada ya miezi 3.
Matokeo yanaonesha kuwa, wagonjwa hao wakifanya mazoezi kwa muda mwingi zaidi, mafuta ndani ya maini yatapungua kwa kiasi kikubwa zaidi.
Watafiti hao hawajagundua uhusiano kati ya kupungua kwa mafuta ya maini na kupungua kwa uzito, lakini inawakumbusha watu kuendelea kufanya mazoezi bila ya kujali kupunguza uzito au la.
0 comments:
Chapisha Maoni