Utafiti uliofanywa na Ujerumani na Uingereza umeonesha kuwa kwa kulinganishwa wagonjwa wa kawaida, wagonjwa wenye tabia ya ulevi wanafariki mapema kwa muda wa wastani wa miaka 7.6.
Chuo kikuu cha Bonn kimetoa taarifa ikisema, wataalam wa chuo hicho walichunguza takwimu za wagonjwa zaidi ya elfu 20 wa miaka 12 na nusu iliyopita katika hospitali kadhaa za Uingereza. Wagonjwa hao walikuwa na maradhi mengi na pia walikuwa na tabia ya ulevi. Takwimu hizo zililinganishwa na wagonjwa wengine laki 2 wasio na tabia ya ulevi.
Matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa, kiwango cha vifo kwa wagonjwa wenye tabia ya ulevi ni asilimia 20 hivi, na kiwango hicho cha wagonjwa wa kawaida ni asilimia 8.3 tu.
Utafiti huo pia unaonesha kuwa kiwango cha wagonjwa hao kupata maradhi ya aina 27 ya ini, kongosho, mufumo wa kupumua, tumbo na mufumo wa neva pia ni cha juu zaidi.
Watafiti wamesema, tabia ya ulevi inaweza kuleta hasara za kisaikolojia na kiafya, hivyo watu wanaosumbuliwa na ulevi wanatakiwa kutafuta msaada mapema zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni