Jumamosi, Machi 26, 2016

CHAI YA KUJANI HUPUNGUZA HATARI YA KIFO

Kituo cha taifa cha utafiti wa saratani cha Japani kimesema, watafiti wa kituo hicho wamethibitisha kuwa kunywa chai ya kijani sio tu kunaweza kupunguza hatari ya kifo, bali pia kunatoa mchango wa kidhahiri katika kupunguza hatari ya magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo na ubongo.
Ili kutambua uhusiano kati ya unywaji wa chai ya kijani na kifo, watafiti walifanya utaifiti wa miaka 19 uliowashirikisha watu elfu 90 wenye umri wa miaka 40 hadi 69. 
Katika miaka 19 iliyopita, watu 12,874 walioshiriki kwenye utafiti huo walifariki. Watafiti waligundua kuwa, kwa watu wanaokunywa vikombe zaidi ya vitano vya chai ya kijani kwa siku kwa wanaume, hatari ya kifo ilipungua kwa asilimia 13 na kwa wanawake kwa asilimia 17. 
Ingawa unywaji wa chai ya kijani hauna uhusiano na vifo vilivyosababishwa na saratani, lakini hatari ya ugonjwa wa moyo ilipungua.
Kwa nini unywaji wa chai ya kijani unaweza kupunguza hatari hiyo? Watafiti wamesema, catechin iliyoko ndani ya chai ya kijani inaweza kurekebisha shinikizo la damu na mafuta mwilini.

0 comments:

Chapisha Maoni