Polisi nchini Kenya wanamzuilia mtu mmoja ambaye amekiri kuwa mwanachama wa kundi la Al shabaab.
Baluku Swaleh, raia wa Uganda alikamatwa kwenye eneo la mpakani la Namanga na inadaiwa alikuwa akielekea nchini Tanzania.
Kamanda wa kitengo cha Ujasusi kaunti ya Kajiado Ngatia Iregi amesema wamenasa picha zinazoonyesha vile Al shabaab inauwa watu nchini Somalia pamoja bendera kutoka kwa mshukiwa huyo.
0 comments:
Chapisha Maoni