Jarida la “Afya ya Usingizi” la Marekani limesema, ikilinganishwa na watu wanaofanya kazi kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, watu wanaobadili zamu mara kwa mara wanakabiliwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata tatizo la usingizi. Hivyo, wako kwenye hatari ya kunenepa au kupata ugonjwa wa umetaboli ukiwemo ugonjwa wa kisukari aina II.
Watafiti wa chuo kikuu cha Wisconsin walitafiti takwimu za afya za watu elfu 1.5, na wakagundua kuwa uzito wa asilimia 48 ya watu wanaobadili zamu mara kwa mara umezidi kiwango cha wastani, ambao ni juu kuliko asilimia 35 ya watu wanaofanya kazi wakati wa mchana. Mbali na hayo, tatizo la usingizi kwa watu hao pia ni kubwa zaidi kulio watu wanaofanya kazi wakati wa mchana.
Utafiti huo pia umegundua kuwa, watu wanaobadili zamu wanaweza kunenepa au kupata ugonjwa wa kisukari wa aina ya II, hasa wale wanaolala kwa muda usiozidi saa 7.
Watafiti wameshauri kufuatilia tatizo la umetaboli la watu wanaobadili zamu.
0 comments:
Chapisha Maoni