Aliyewahi kuwa golikipa wa Simba SC ya Tanzania na timu ya taifa ya Uganda, Abel Dhaira amefariki dunia na miaka 28 kwa ugojwa wa saratani ya utumbo huko Iceland ambako alikuwa akitibiwa.
Dkt. Bernard Ogwel, kutoka Federation of Uganda Football Associations (Fufa), ameithibitisha kutokea kwa kifo hicho leo.
"hii ni huzuni sana kwa familia yake na Uganda kama nchi," alisema Ogwel .
Mwishoni kabla ya mauti yake Dhaira alikuwa akicheza mpira katika ligi kuu ya Iceland katika klabu ya IBV na baadae kuzidiwa na maradhi ya saratani katika miezi ya hivi karibuni.
Dhaira pia aliwahi kuzichezea timu za Express FC ya ligi kuu ya Uganda, kabla ya kujiunga na AS Vita ya Congo DR NA BAADAE Simba SC YA Tanzania.
FICHUO BLOG
0 comments:
Chapisha Maoni