Jumamosi, Machi 26, 2016

JUMLA YA WAFANYA KAZI HEWA 515 WAMEGUNDULIKA TOKA MIKOA MITATU YA KIGOMA, DODOMA NA SINGIDA

Siku 15 zilizotolewa na Rais Magufuli kwa Wakuu Wapya wa Mikoa kuhakikisha wanawabainisha na kuwaondoa wafanyakazi hewa zimeanza kutoa picha kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa nchini.
Mpaka sasa imebainika kuna wafanyakazi 515 katika mikoa mitatu ambayo ni Kigoma (169), Dodoma (144) na Singida (202).
Taswira hii inaonyesha jinsi ambavyo tatizo la wafanyakazi hewa linaweza kuwa ni kubwa zaidi ya ilivyofikiriwa hasa ikichukuliwa limekuwepo kwa muda mrefu huku mamilioni ya pesa za walipa kodi yakienda kwenye mifuko ya wajanja wachache.
Inakadiriwa serikali ina wafanyakazi zaidi 500,000 na inalipa mishahara takriban Sh. bilioni 549 kwa mwezi, ambayo kati ya fedha hizo kuna malipo ya wafanyakazi hewa.
Katika repoti yake ya mwaka 2013/14, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alibainisha kuna zaidi ya Sh141.4bn zimelipwa kwa wafanyakazi hewa katika mwaka wa fedha.

0 comments:

Chapisha Maoni