Jumamosi, Februari 27, 2016

WANAWAKE WALIOJIFUNGUA WANAKABILIWA NA HATARI NDOGO ZAIDI YA KIFO

Utafiti mpya unaonesha kuwa uzazi unawezekana kuwa na uhusiano na hatari ya kufa kwa wanawake inayosababishwa na maradhi. Takwimu zinaonesha kuwa wanawake waliojifungua wanakabiliwa na hatari ndogo zaidi ya kufariki kuliko wanawake wasiozaa.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Imperial cha Uingereza walitafiti uhusiano kati ya uzazi na hatari ya kifo inayosababishwa na saratani ya matiti, kiharusi, na magonjwa ya moyo. Watafiti hao walichunguza takwimu za wanawake zaidi ya laki 3.2 kutoka nchi 10 ambao umri wao wa wastani ni miaka 50. 
Kila mwanamke aliangaliwa kwa miaka 12 katika kipindi hiki, ambapo elfu 14 kati yao walifariki. Vifo 5,938 vilitokana na saratani, na vifo 2,404 vilisababishwa na maradhi ya mfumo wa damu. 
Kwa upande wa saratani, utafiti huo unaonesha kuwa kiwango cha kupata saratani kwa wanawake waliojifungua pia ni kidogo, hasa wanawake waliozaa watoto wawili au watatu.

0 comments:

Chapisha Maoni