Jumamosi, Februari 27, 2016

SHABIKI MTOTO WA MESSI ATUNUKIWA NA MCHEZAJI HUYO

Shabiki mtoto wa Lionel Messi, Murtaza Ahmadi mwenye miaka mitano kutoka Afghanistan aliyeonekana na jezi ya mfuko wa plastiki amepata jezi zuri kutoka kwa mchezaji huyo wa Argentina.
Murtaza Ahmadi, alitumiwa jezi hilo, lililokuwa limetiwa saini ya mchezaji huyo pamoja na mpira.
Msako wa mtoto huyo katika mtandao ulisababishwa na picha moja ilioenea katika mitandao ikimuonyesha amevaa fulana ya plastiki ya Messi.

0 comments:

Chapisha Maoni