Wafanya upasuaji katika kliniki ya Cleveland wamefanya upasuaji wa kwanza wa kupandikiza mfuko wa uzazi nchini Marekani,kwa kutumia mfuko wa uzazi kutoka kwa mfadhili wa viungo aliyekufa,hospitali ilisema.
Mgonjwa mwenye umri wa miaka 26 ambaye hakutaka kutambuliwa hadharani alikuwa katika hali ya utulivu baada ya upasuaji uliochukua masaa tisa siku ya Jumatano,kliniki hiyo ya Cleveland ilisema katika taarifa.
Hospitali hiyo ilisema kuwa itajaribu upasuaji huu kwa wanawake wengine kumi walio tasa,ambao aidha walizaliwa bila mfuko wa uzazi au wamepata uharibufi wa mfuko wa uzazi ambao hauwezi rekebishwa.
Utasa huathiri asilimia tatu hadi asilimia tano ya wanawake duniani kote,na upandikizaji huu wa mfuko wa uzazi unapatia wagonjwa hao nafasi ya kuweza kubeba mimba tena.
0 comments:
Chapisha Maoni