Jumapili, Februari 14, 2016

WANAMUZIKI WANNE WA BENDI YA VIOLA BEACH WAFARIKI AJALINI

Taarifa iliyotufikia mezani kwetu ni kwamba wanamuziki  wanne wa bendi ya ‪‎Viola‬ Beach kutoka Uingereza wamefariki dunia jana kwenye ajali ya barabarani iliyotokea nchini Sweden.
Ofisi ya mambo ya kigeni ya Uingereza imesema wanne hao ni Kris Leonard, River Reeves, Tomas Lowe na Jack Dakin.
Meneja wao Craig Tarry pia anaaminika kuwa amefariki kwenye ajali hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni