Jumatatu, Februari 15, 2016

KULA NYAMA AU SAMAKI KABLA YA WALI ITAKUSAIDIA

Watafiti wa taasisi ya matibabu ya Kansai ya Japan wamegundua kuwa, watu wanapokula chakula, kula nyama au samaki kabla ya wali kunapunguza kasi ya usakaji wa tumbo na kuzuia ongezeko la sukari katika damu baada ya mlo.
Watafiti wamefanya majaribio kwa wagonjwa 12 wa kisukari aina ya II na watu 10 wazima, na kulinganisha katika hali ya kula wali kwanza na hali ya kula samaki na nyama ya ng’ombe kabla ya kula watu, jinsi sukari katika damu inavyobadilika ndani ya saa 4.
Matokeo yanaonesha kula samaki kwanza, ongezeko la sukari katika damu linazuiliwa kwa asilimia 30 ikilinganishwa na kula wali kwanza, na kula nyama ya ng’ombe kwanza, ongezeko la sukari katika damu lilizuiliwa kwa asilimia 40 ikilinganishwa na kula wali kwanza. Watafiti wanasema, kubadilisha utaratibu wa kula chakula kutasaidia kukinga na kutibu ugonjwa wa kisukari.

0 comments:

Chapisha Maoni