Serikali kupitia wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia na watoto imesema itaanza kusambaza madaktari bingwa maeneo ya pembezoni ukiwemo mkoa wa Ruvuma kuanzia mwezi julai mwaka huu ili kuwaondolea wananchi adha ya kufuata huduma za madaktari bingwa mbali na maeneo yao.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii jinsia na watoto mjini Songea, Dkt Hamis Kigwangala baadaya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma na kituo cha afya cha Mjimwema kilichopo mjini Songea huku akiitaka mikoa ya pembezoni ukiwemo mkoa wa Ruvuma kuweka mazingira ya kuwavutia madaktari bingwa kufanya kazi katika mikoa yao.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu amesema kuwa mkoa huo umeridhishwa na staili ya ziara ya kushtukiza na kwamba wanajitahidi kuboresha vituo vya afya vya Mjimwema Songea, Madaba na cha wilaya ya Namtumbo ili vipandishwe hadhi kuwa hospitali za wilaya.
Katika hatua nyingine Dkt Kigwangala ametoa miezi mitatu kwa hospitali ya Kibena mkoani Njombe kurekebisha mapungufu yaliyopo ikwepo maabala vinginevyo ataifunga hospitali hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni