Rais wa Jamhurui ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa takriban watoto milioni 1.3 wamejiunga na shule tangu kuanzishwa kwa mpango wa elimu ya bure.
Hata hivyo Rais Magufuli alisema kuwa mpango huo wa elimu ya bure inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa madarasa na madawati ya kusomea. Alisema kuwa serikali yake imetenga dola milioni 69 kusaidia katika utoaji wa elimu ya bure kati ya mwezi Januari mwaka huu na Juni mwaka ujao. Rais Magufuli alisema serikali yake itaipa kipaumbele elimu ya bure katika sera zake.
0 comments:
Chapisha Maoni