Jumatano, Februari 10, 2016

UKO TAYARI KWA COLLABO YA CHRISTIAN BELLA NA JOH MAKINI?

Ngoma ya Nagharamia ya Christian Bella aliyomshirikisha Ali Kiba ikiendelea kutamba mjini, msanii huyo ameamua kuipua ngoma nyingine iitwayo Natamani Nijue ambayo jana alitarajia kumalizia ‘ku-shoot’ video yake.
Safari hii Bella ameamua kwenda mbali kwa kuwashirikisha memba wa Weusi ambao ni Joh Makini na G Nako katika wimbo huo ambao bado hajapanga siku maalum ya kuuachia ingawa amedokeza kuwa inaweza kuwa ndani ya mwezi huu au Machi.
Kama kawaida ya Bella wimbo huo upo kwenye maudhui ya mapenzi ingawa ndani yake kutakuwa na wasanii hao wa Hip Hop, lakini pia utakuwa kwenye ladha na mahadhi ya Rhumba na R&B.
“Ndiyo ngoma yangu mpya inayofuata, tupo kwenye hatua za mwisho za kumalizia ‘kushoot’ video yake, Jumanne hii (jana) tutamaliza kila kitu na sijajua hasa lini naweza kuiachia lakini kama haitakuwa Februari hii basi itakuwa Machi.
“Ndani wapo kina Joh Makini na G, natarajia kazi itapokewa vizuri kama zilivyokuwa za huko nyuma, siwezi kusema kwamba itakuwa bora zaidi ya nyingine kwa sababu kila shabiki ana upokeaji wake kulingana na ngoma ilivyomgusa lakini ni nzuri kwa kweli,” alisema Bella.

0 comments:

Chapisha Maoni