Jumatatu, Februari 22, 2016

NJIA MPYA YAZINDULIWA KUZUIA KUENEA KWA SELI ZA SARATANI

Watafiti wa Uingereza na Denmark wamezindua njia mpya inayoweza kuzuia seli za saratani katika sehemu moja zisienee mwilini. Katika siku ya baadaya tiba moya itazinduliwa juu ya msingi wa njia hiyo.
Baada ya kutokea uvimbe kwenye sehemu ya mwili, seli za uvimbe zinaweza kuzifanya seli zilizoko karibu kuwa ngumu, hivyo seli za saratani zinaweza kuingia katika damu na kuenea katika sehemu nyingine za mwili. 
Watafiti wamegundua kuwa matumizi ya dawa moja ya majaribio inaweza kuzuia mfumo wa kuenea kwa seli za saratani. Katika majaribio ya wanyama, panya waliopata saratani walipotumia dawa hiyo, kiwango cha kuenea kwa seli za saratani kilipungua kwa kiasi kikubwa.

0 comments:

Chapisha Maoni