Jumatatu, Februari 22, 2016

IDADI YA WABUNGE MASHOGA UINGEREZA YAVUNJA REKODI YA DUNIA

Idadi ya wabunge wanaoingiliana kinyume na maumbile nchini Uingereza imeongezeka baada ya wabunge wengine wawili kutangaza hadharani kwamba wanajihusisha na vitendo hivyo vichafu.
Gazeti la Daily Mail limeandika kuwa wabunge Hannah Bardell na Nia Griffith wa Uingereza wamejitangaza hadharani wiki hii kwamba wanafanya maingiliano kinyume na maumbile. Kwa sasa Uingereza ina wabunge 35 mashoga wanaoifanya nchi hiyo kuweka rekodi ya kimataifa ya kuwa na idadi kubwa zaidi ya wabunge wanaoingiliana kinyume na maumbile.
Mbunge wa kwanza kujitangaza hadharani kwamba anajihusisha na vitendo vichafu vya liwati alikuwa Lord Criss Smith katika muongo wa 1980. Mwaka 1989 Lord Smith aliteuliwa kuwa wazii katika serikali ya Tony Blaire na kuwa waziri wa kwanza shoga katika serikali ya nchi hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni