Jumatatu, Februari 22, 2016

JE, KWA NINI WATU WENGI WANASIKIA USINGIZI MARA KWA MARA?

Ingawa watu wengi wanalala kwa muda mrefu, lakini bado wanasikia usingizi mara kwa mara. Tovuti moja ya Ujerumani imeorodhesha vyanzo vinane vikuu vinavyokusababisha hali hiyo.
1. Tatizo la dundumio
Dundumio inaweza kuzalisha homoni za kurekebisha metaboli. Kama dundumio lina tatizo, uwezo wake utapungua na haiwezi kuzalisha homoni ya kutosha, hivyo watu watasikia usingizi. 
2. Ukosefu wa madini ya chuma katika damu
Wanawake wengi wanakosa madini ya chuma mwilini, ambao unaweza kuwafanya wasikie uchovu na usingizi.
3. Kunywa maji kidogo
Utafiti unaonesha kuwa watu wasiokunywa maji sana hawawezi kulala vizuri, hivyo mchana watasikia usingizi.
4. Ugonjwa wa kisukari wa aina ya pili
Watu wenye ugonjwa wa kisukari wa aina ya pili wanapata tatizo katika mchakato wa insulini kubadilisha sukari kuwa nishati, hivyo watajikia usingizi na uchovu.
5. Ukosefu wa mazoezi
Ni rahisi kwa watu wasiofanya mazoezi kuona uchovu na usingizi.
6. Ukosefu wa vitamin B-12
7. Kunywa kahawa na chai katika muda usiofaa
Unapokunywa kahawa au chai wakati wa mchana, labda utakosa usingizi wakati wa usiku, na siku inayofuata utasikia usingizi tena, hivyo utaingia katika mzunguko mbaya.

0 comments:

Chapisha Maoni