Jumamosi, Februari 27, 2016

MTAFARUKU WA MACHINGA NA JIJI LEO MBEYA

Hali ya usalama hapa jijini Mbeya haikuwa nzuri baada ya wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) eneo la Kabwe, Mbeya kufanya vurugu kwa kuchoma matairi barabarani katika eneo hilo wakipinga hatua ya serikali kubomoa vibanda vyao.
Vibanda hivyo vilibomolewa usiku wa kuamkia leo. 
Wafanyabiashara walipofika Kabwe na kuona wamebomolewa, ndipo walipofanya vurugu.
Vurugu hizo zimepungua sasa baada ya jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya kuwatawanya wafanyabiashara hao.

0 comments:

Chapisha Maoni