Jumamosi, Februari 27, 2016

MAREKANI KUONGEZA UMRI HALALI WA KUNUNUA SIGARA HADI KUFIKIA MIAKA 21

Taasisi ya matibabu ya watoto ya Marekani imeishauri serikali ya Marekani kuongeza umri halali wa kununua sigara hadi kufikia miaka 21.
Taasisi hiyo imesema, uvutaji wa sigara ni tishio kubwa kwa afya, na ubongo wa watoto na vijana uko katika kipindi cha ukuaji, ambao unaweza kuharibiwa na nikotini.
Mbali na kupendekeza kuongeza umri wa kununua sigara, taasisi hiyo pia ilipendekeza kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika ofisi, baa, mikahawa na hospitali.
Matangazo yoyote kuhusu tumbaku yanayoweza kugusiana na vijana pia yanatakiwa kupigwa marufuku. 
Taasisi hiyo imeona kuwa, sigara ya kielektroniki pia inatumiwa sana na vijana, serikali inatakiwa kudhibiti sigara hiyo sawa na sigara ya kawaida.
Katika miaka ya karibuni, kutokana na ushuru mkubwa wa tumbaku, udhibiti mkali wa uvutaji wa sigara na kuibuka kwa sigara ya kielektroniki, kiwango cha uvutaji wa sigara wa wamarekani kinaendelea kupungua.

0 comments:

Chapisha Maoni