Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo ijumaa Februari 26, 2016 ameongea na waandishi wa habari kuhusu kadhia ya baadhi ya mawaziri wa serikali ya awamu ya tano kushindwa kuresha fomu za hati ya mali ya wanazomiliki. Kwanza alielezea sekretarieti ya maadili na nini wajibu wake ikiwemo kufatilia maadali ya viongozi wa umma na sheria inayowataka viongozi husika kutoa tamko la mali ndani ya siku thelathini tangu uteuzi wao.
Majawaliwa: Viongozi wanaoshindwa kutoa tamko katika kipindi kilichowekwa kwa mujibu wa sheria wanawajibika kutoa maelezo ya sababu za msingi za kushindwa kwao kuwasilisha fomu hizo za tamko la rasilimali na madeni waliyonayo.
Endapo maelezo hayo hayatakuwa na sababu za msingi, hatua zaidi za kisheria huwa zinachukuliwa. Aidha viongozi wa umma wanawajibika kusaini hati za maadili, ahadi ya uadilifu kwa viongozi wote wa umma. Zoezi hili lilianza mwaka 2015 na ni endelevu na lilikuwa na lengo la commitment ya kiongozi juu ya uadilifu wake wakati wote anapokuwa kiongozi wa umma na tayari watumishi wengi wa umma wanaendelea kuzijaza fomu hizo na ndio msingi wa uwajibikaji katika sekta ya umma.
Kwa misingi hiyo, mawaziri bado wanaendelea na zoezi hilo lakini pia mtu toka alipoteuliwa. Fomu hizo walishakabidhiwa na wanawajibika kurudisha tume.
Jana nilikabidhiwa majina ya mawaziri na manaibu mawaziri ambao hawakuweza kurudisha fomu zote mbili au fomu moja. Na alikuwa analikuwa anatakiwa pia watoe tamko la rasilimali walizonazo na madeni waliyonayo na fomu hizo walitakiwa kurejesha kwa kamishna.
Mhashimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ameelekeza kwamba waziri na manaibu waziri wote ambao hawajajaza tamko la rasilimali na madeni, ifikapo leo Ijumaa saa kumi na mbili jioni wawe wameshajaza na kurejesha fomu hizo ofisi ya tume ya maadili hapa Dar es Salaam.
Kwa waziri yeyote ambae atashindwa kutekeleza agizo hilo atakua amejiondoa mwenyewe kwa majukumu aliyonayo ya uwaziri au unaibu waziri. Na mheshimiwa Rais ameelekeza lazima wasomwe ili popote walipo warudi na watekeleze hivyo na ofisi yangu itasimamia kwa ukaribu kuona kwamba fomu hizo zinapatikana ifikapo saa 12.
Nao ni wafuatao, kundi la mawaziri
Charles Kitwanga(Waziri wa mambo ya ndani, yeye hajarejesha fomu zote mbili)
January Makmba (Hajarejesha fomu zote mbili)
Dr Augustine Mahiga (Waziri wa mambo ya nje, Fomu moja ya maadili)
Prof Ndalichako (Fomu moja ya tamko)
Manaibu
Luhaga Mpina (Mazingira na muungano, hajajaza fomu zote mbili)
0 comments:
Chapisha Maoni