RAPPA na muigizaji kutoka nchini Marekani, Earl Simmons, “DMX” jana jioni alikimbizwa hospitali baada ya kuanguka sakafuni akiwa nyumbani kwake huko Ramada Yonkers, New York.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo hilo ni kwamba DMX kabla ya kuanguka alianza kulalamika kuwa anasijisikia matatizo katika upumuaji na maumivu kifuani.
Baada ya kuanguka, gari la kubebea wagonjwa lilifika eneo hilo na kumuwahisha hospitali iliyo karibu na nyumbani kwake ambapo anaendelea na matibabu.
Msanii huyo ana historia ya kusumbuliwa na ugonjwa wa pumu (asthma) na huenda ndiyo chanzo cha kuanguka kwake jana.
0 comments:
Chapisha Maoni