Jeshi ni sehemu muhimu ya nchi na usalama wake. Kila mwaka nchi hutenga bajeti kwa ajili ya kuimarisha majeshi yake. Nchi nyingi duniani huchukua tahadhari za kiusalama kwa kuimarisha majeshi yake kulinganisha na nchi nyingine zinavyofanya. Nchi hizo hufanya hivyo kwa kumiliki idadi kubwa ya wanajeshi, kuboresha teknolojia ya kijeshi, kutoa mafunzo na kutengeneza propaganda za kidiplomasia ili kuwaogopesha maadui wao wa kiusalama.
Ngoja tuangalie majeshi kumi (Top 10) hatari duniani kwa sasa na bajeti zake;
10: JAPAN
Japan ilikuwa moja ya nchi vinara katika Vita ya Pili ya Dunia (WW2) iliyomalizika mwaka 1945. Cha kufurahisha, baada ya vita hiyo, Japan iliingia kwenye mkataba wa amani na kukubaliana kuwa na jeshi la kawaida lakini kufuatia kukua kwa Jeshi la China ndipo ikaanza kupanua tena jeshi lake ikiweka ngome za kijeshi kwenye visiwa vyake.
Bajeti ya Jeshi la Japan imekuwa ikiongezeka kila mwaka hadi kufikia Dola za Kimarekani bilioni 49.
Jeshi hilo lina zaidi ya wanajeshi 247,000 waliopo kazini na zaidi 60,000 wa akiba. Lina ndege za kivita zipatazo 1,595 na meli 131.
9: KOREA KUSINI
Korea Kusini wanashirikiana mpaka na Korea Kaskazini ambao nao wapo vizuri kijeshi. Ili kukabiliana na majeshi makubwa ya China and Japan, Korea Kusini imekuwa ikiongeza bajeti ya jeshi lake hadi kufikia dola bilioni 34. Lina wanajeshi waliopo kazini 640,000 na wengine wa akiba 2,900,000. Lina ndege kubwa za kivita 1,393 na meli za kijeshi 166.
8: UTURUKI
Labda ni kwa sababu ya kushirikiana kupambana na kundi korofi la kigaidi la Islamic State linalotishia amani duniani ndiyo maana ni kubwa na linaogopeka zaidi. Limeongeza bajeti yake kwa 10% hadi kufikia dola bilioni 18.
Lina wanajeshi wapatao 660,000 walioko kazini na wa akiba. Pia lina ndege za kivita 1,000 na silaha za nchi kavu 16,000 likiwa lina ushirikiano mkubwa na lile la Marekani.
7: UJERUMANI
Miongoni mwa nchi zenye majeshi hatari duniani ni Ujerumani. Linatengewa bajeti ya dola bilioni 45, japokuwa linaonekana kushuka katika miaka ya hivi karibuni labda kwa sababu kizazi cha sasa nchini humo hakipendi mambo ya vita na watu wengi wanaogopa kujiunga na jeshi hilo.
Lina wanajeshi 183,000 walioko kazini na 145,000 wa akiba likiwa na ndege za kivita 710 na silaha za nchi kavu zaidi ya 5,000.
6: UFARANSA
Katika miaka ya hivi karibuni, Ufaransa imepunguza bajeti ya jeshi lake hilo kwa 10%. Bajeti yake inafikia dola bilioni 43 kwa mwaka. Lina wanajeshi 220,000 waliopo kazini na 500,000 wa akiba. Pia lina ndege za kivita 1,000 na vifaa vya nchi kavu 9,000.
UINGEREZAWaajeshi wa Uingereza.
5: UINGEREZA
Uingereza ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) ambao wapo kwenye mkakata wa kupunguza wanajeshi wake kwa 20%.
Bajeti ya jeshi lake hatari ni dola bilioni 54 kwa mwaka likiwa na wanajeshi 205,000, ndege za kivita 908 na meli 66.
4: INDIA
Jeshi lake lina jumla ya ‘wajeda’ milioni 3.5, wakiwemo milioni 1.325 waliopo kazini na wengine ni wa akiba. Lina magari ya kivita 16,000 na ndege 1,785 pamoja na silaha za nyuklia. Bajeti yake ni dola bilioni 46.
3: CHINA
Bajeti ya Jeshi la China inafikia dola bilioni 126 likiwa na wanajeshi milioni 2.285 waliopo kazini na milioni 2.3 wa akiba. Ni moja ya majeshi makubwa kwa sasa duniani likiwa katika Tatu Bora.
Lina vifaa vya kivita vya nchi kavu 25,000 na ndege 2,800. Pia lina silaha za nyuklia 300.
2: URUSI
Bajeti ya jeshi hatari la Urusi ni dola bilioni 76.6 ambayo inatarajiwa kuongezwa kwa 44%.
Tangu alipoichukua Urusi, Rais Vladimir Putin mwaka 2000, nchi hiyo imekuwa moto wa kuotea mbali katika masuala ya kijeshi. Lina wanajeshi 766,000 waliopo kazini na milioni 2.5 wa akiba. Urusi inaongoza kwa silaha za kivita zikiwemo za nyuklia zipatazo 8,500.
Scouts with the 82nd Airborne Division’s 1st Brigade Combat Team fire on a line during a course in advanced rifle marksmanship March 21-24, 2011, at Fort Bragg, N.C. The weeklong course emphasized adapting to battlefield problems by knowing one’s tools and capabilities. (U.S. Army photo by Sgt. Michael J. MacLeod)
1: MAREKANI
Jeshi kinara la Marekani linatengewa bajeti ya dola bilioni 612.5. Hakuna jeshi lenye bajeti kama hiyo duniani. Lina wanajeshi milioni 1.4 waliopo kazini na 800,000 wa akiba. Hawa jamaa ni wabaya kwa ndege, meli na manowari za kivita. Pia lina silaha za nyuklia 7,500. Kama ulikuwa hujui ndilo jeshi namba moja duniani tangu Vita ya Pili ya Dunia iliyomalizika mwaka 1945.
Nchi kama Urusi na China zinangoja sana kwa jeshi la Marekani kutokana na kuwa na mbinu na teknolojia ya hali ya juu ya kijeshi.
GPL
0 comments:
Chapisha Maoni