Tariban wakimbizi 10,wakiwa pamoja na watoto watano waliaga dunia baada ya mashua waliokuwa ndani kuzama katika Bahari la Aegean mapema Jumamosi (jana) walipokuwa wakielekea katika kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos, vyombo vya habari vya Uturuki vilitoa taarifa hiyo.
Mashua hiyo ilikuwa imebeba takriban wakimbizi 53 kutoka Syria,Afghanistan na Myanmar ilipozama katika pwani la Bademli,magharibi mwa Uturuki muda mfupi tu baada ya kuondoka kutoka Ayvacik katika wilaya ya Canakkale.
Walinzi wa pwani waliwaokoa wakimbizi 43 kutoka baharini,ripoti hiyo ilisema.




0 comments:
Chapisha Maoni