Jumanne, Januari 26, 2016

UWEKEZAJI WAPUNGUA AFRIKA

Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja barani Afrika ulipungua mwaka jana kwa asilimia 31 ambayo ni sawa na dola bilioni 38.
Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya awali ya makadirio ya uwekezaji mwaka 2015 kimataifa iliyotolewa na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD, mwezi huu wa Januari ambapo kwa mujibu wa ripoti hiyo, mataifa mengi ya Afrika yameshuhudia kushuka kwa uwekezaji wa kigeni hususan yale ya kusini mwa jangwa la Sahara.
Katibu Mkuu wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi akizungumza na waandishi habari baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo ametaja sababu za mataifa ya Afrika ya kusini mwa jangwa la Sahara kukumbwa na hali hiyo.
Kituyi ameongeza kuwa nchi za Afrika zilizoko kaskazini kama vile Misri yalishuhudia kuongezeka kwa uwekezaji huku Marekani ndio kidedea katika nchi kumi zilizopata uwekezaji wa juu zaidi, nyingine ni China, Uingereza na Ufaransa ikichukua nafasi ya kumi.

0 comments:

Chapisha Maoni