Jumatatu, Januari 25, 2016

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG'ATWA NA NYOKA

Nyoka ni wanyama hatari pale wanapomg’ata mtu, wanaweza kusababisha kifo papo hapo au baada ya muda.
Huduma ya Kwanza:
1.Hakikisha mgonjwa anatulia, asihangaike wala kutembea tembea.
2. Mlaze chini. Asiinue sehemu iliyong’atwa juu zaidi ya usawa wa moyo. Hii itasaidia kupunguza sumu kusambaa mwilini.
3. Ondoa vitu vinavyobana kama pete au nguo za kubana kwenye sehemu iliyong’atwa kwani sehemu hiyo inaweza kuvimba.
4. Angalia hali ya mgonjwa: joto la mwili, mapigo ya moyo na upumuaji. Kama anakuwa wa baridi malze chali na kisha umfunike kwa blanketii
5.Muwahishe kituo cha afya
Kama nyoka aliyemng’ata yupo (amekufa) nenda naye hospitali pia.

0 comments:

Chapisha Maoni