Mwanasayansi Dk Derek Lee amegundua twiga albino kwenye hifadhi ya mbuga ya Tarangire iliyopo katika Mkoa wa Arusha nchini Tanzania.
Mtafiti huyo Dk Derek Lee, alipiga picha mbalimbali zikiwa zinamwonyesha mnyama huyo akiwa katika kundi kubwa la twiga, huku akiwa na rangi ya kipekee ikilinganishwa na twiga wengine duniani.
Dk Lee, alimgundua twiga huyo wakati akifanya utafiti kwenye mbuga hiyo na nyingine za wanyama za barani Afrika,
Taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari nchini Uingereza kupitia gazeti la Dailymail zimeeleza kuwa, twiga huyo adimu kupatikana duniani iwapo atahifadhiwa atakuwa kivutio cha pekee katika mbuga hiyo .
0 comments:
Chapisha Maoni