Jumanne, Januari 26, 2016

SIMBACHAWENE AMPIGA CHINI MKURUGENZI DODOMA

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, George Simbachawene, amemvua madaraka Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma, Augustino Kapinga kwa kushindwa kusimamia watumishi wa chini yake.
Waziri Simbachawene alifikia uamuzi huo, baada ya usimamizi duni wa Kapinga kusababisha wafanyakazi hao kutoa maagizo ya kuchangisha michango ambayo Rais aliizuia.
Mbali na Kapinga, Waziri Simbachawene jana alimsimamisha Ofisa elimu vifaa na takwimu-wa msingi katika Manispaa hiyo, Josephine Akimu kwa kudharau maelekezo ya kiongozi wake na kusaini barua kwa niaba ya mkurugenzi huku akitumia jina la Ofisa Elimu, Scola Kapinga ambaye pia amepewa onyo kali .

0 comments:

Chapisha Maoni