Alhamisi, Januari 28, 2016

UTAFITI WAONESHA UKUAJI WA VIRUSI VYA UKIMWI MWILINI UNATEGEMEA KUGUSIANA KWA SELI

Watafiti wa Japani wamegundua kuwa seli inayoambukizwa na virusi vya UKIMWI inaambukiza seli nyingine kupitia njia ya kugusana.
Wamegundua kuwa hii ni njia kuu ya ukuaji wa virusi vya UKIMWI ndani ya mwili wa binadamu. Watafiti wanaona kuwa kama maambukizi kati ya seli yanaweza kuzuiliwa, matibabu ya ugonjwa wa UKIMWI yataboreka.
Utafiti wa awali unaonesha kuwa virusi vya UKIMWI vina njia mbili za kuziambukiza seli, ya kwanza ni virusi vinaondoka kwenye seli inayoambukizwa na UKIMWI na kuingia katika majimaji ya mwili wa binadamu ili kuziambukuza seli nyingine, ya pili ni virusi vinaambukiza seli nyingine kupitia kugusana kwa seli.
Jaribio lililofanywa na watafiti kutoka chuo kikuu cha Kyushu, chuo kikuu cha Kyoto na Chuo kikuu cha Tokyo linaonesha kuwa kiwango cha seli zinaambukizwa virusi kupitia njia ya kugusiana ni asilimia 60 ya seli zote zinazoambukizwa. Na seli zinapogusiana, kasi ya maambukizi ni mara 3.9 ya kasi ya hali isiyo ya kugusiana kwa seli.
Watafiti wataendelea kutafuta protini inayosaidia maambukizi ya virusi vya UKIMWI, ili kupata matibabu mapya ya ugonjwa huo.

0 comments:

Chapisha Maoni