Alhamisi, Januari 28, 2016

MAUA YAFANANAYO NA KIMA


Katika misitu ya mvua ya Amerika yenye mazingira ya kipekee, kuna mimea mingi ya ajabu, ikiwemo okidi ya kima (Dracula simia).
Maua ya okidi ya kima yanafanana sana na uso wa kima. Petali za maua zimeunda uso, macho na mdomo, na stameni ina umbo la pua. Maua hayo yanaiga uso wa kima ili kuwavutia kima kuichavusha? Bila shaka haiwezekani.
Mwaka 2010, wataalamu watatu wa biolojia wa Marekani walitoa tasnifu kuhusu uchavushaji wa okidi za jeni ya Dracula, na kugundua siri ya okidi hizi.
Ukweli ni kwamba maua ya okidi za jeni ya Dracula yanaiga uyoga badala ya kima, hata yanatoa harufu ya uyoga, ili kuwavutia inzi wanaopenda kula uyoga kuyachavusha. Stameni ya kipekee inawafanya inzi kugandamizwa na chembe za chavuo kwa urahisi.
Katika mazingira ya kimaumbile, mfano kati ya viumbe tofauti si nadra, kwa kawaida vinaiga viumbe vingine kwa malengo maalum. Lakini kwa okidi ya kima, sura yake inayofanana na uso wa kima kweli ni jambo lililotokea kwa bahati.

0 comments:

Chapisha Maoni