Serikali ya Marekani na ile ya Uchina inanuia kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa biashara haramu ya pembe za ndovu kutoka mataifa ya Afrika inapigwa marufuku katika nchi hizo mbili, Waziri wa Mambo ya Ndani Sally Jewell alisema siku ya Jumatano.
"Nilitembelea nchi ya China na nilikuwa na majadiliano na makamu wa Rais Wang Yang, kuhusu hatua zitakazochukuliwa kuhakikisha kuwa biashara haramu vya pembe ya ndovu vinakomeshwa",Jewell aliambia mkutano wa wanahabari, ikiwa ni siku yake ya tano na ya mwisho ya ziara yake nchini Kenya.
Jewell alisema Uchina, Marekani na Kenya itachukua hatua ya pamoja yakupunguza biashara ya wanyamapori haramu.
0 comments:
Chapisha Maoni