Jumatano, Januari 27, 2016

KUTOKA KATIKA KURASA ZA MICHEZO ULAYA LEO

Manchester United wana wasiwasi kuwa meneja msaidizi Ryan Giggs huenda akaondoka baada ya kuwepo Old Trafford kwa miaka 28, iwapo hatofikiriwa kuchukua nafasi ya Louis van Gaal (Daily Mirror), Van Gaal hatojiuzulu kumpa nafasi Jose Mourinho au kocha yeyote (Manchester Evening News), kipa wa Everton Tim Howard, 36, anafanya mazungumzo "mazito" na klabu ya Colorado Rapids ya Marekani na huenda akaondoka Goodison Park baada ya miaka 10 (NBC Sports), Tottenham watarejea tena West Brom na dau la pauni milioni 18 kumtaka Saido Berahino, 22 (Daily Mirror), meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anafikiriwa na Chelsea kama mmoja wa makocha kwenda kujiunga Stamford Bridge msimu ujao (Independent), Fulham wamewaambia Tottenham kuwa hawataki kumuuza mshambuliaji wao, Moussa Dembele, 19, lakini Spurs huenda wakakamilisha usajili huo na kumrejesha Fulham kwa mkopo (Guardian), Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Corinthians Alexandre Pato, 26, kwa mkopo wa miezi sita wakiwa na nafasi ya kumsajili moja kwa moja mwisho wa msimu (London Evening Standard), Chelsea watataka angalau pauni milioni 80, iwapo watamuuza Eden Hazard, 25, mwisho wa msimu (Sun), Chelsea huenda wakakabiliwa na adhabu ya kutosajili, baada ya kiungo wao Betrand Traore kuichezea timu yao ya chini ya miaka 18 wakati akiwa bado mdogo sana kusajiliwa hatua ambayo ni kuvunja kanuni za Fifa (London Evening News), lakini Chelsea wana uhakika hawakuvunja kanuni yoyote kwa sababu mchezo huo haukuwa wa ushindani (Guardian), Chelsea wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Robin van Persie, 32, kutoka Fernabahce (Daily Express), Sunderland watapanda dau tena kwa Swansea na kutoa zaidi ya pauni milioni 10 kumsajili Andre Ayew, 26, na pia kuwapa Fabio Borini, 24 (TalkSport), lakini Swansea wanasisitiza kuwa mfungaji wao bora, Ayew, hauzwi (South Wales Evening Post), Swansea wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Napoli, Jonathan de Guzman, 28, aliyeichezea Swansea kwa mkopo kati ya mwaka 2012 na 2014 (Daily Express), mshambuliaji wa Liverpool, Jerome Sinclair, 19, ameiambia klabu yake kuwa anataka kuondoka, huku Watford wakiwa na matumaini ya kumsajili (Telegraph), Leicester City wameongeza dau lao kutoka pauni milioni 7.95 hadi 10, kumtaka mshambuliaji wa Sampdoria Eder, 29, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Inter Milan (Daily Mail), meneja wa Leicester Claudio Ranieri pia anamnyatia mshambuliaji wa CSKA Moscow, Ahmed Musa, 23 (Daily Mirror), Liverpool wamepewa "moyo" na kocha wa Shakhtar Donetsk kumsajili Alex Teixeira, 26, (Daily Express), dau la Arsenal la kumsajili kiungo wa Napoli, Jorginho, 24, limekataliwa lakini huenda Gunners wakarejea tena mwisho wa msimu (TuttoMercatoWeb), Necastle wameambiwa na Chelsea watoe pauni milioni 12 kumsajili Loic Remy, 29 (Daily Mail), Newcastle wanafikiria kumchukua Remy kwa Mkopo (Evening Chronicle), beki wa Arsenal anayecheza West Ham kwa mkopo, Carl Jenkinson huenda akakosa kucheza hadi mwisho wa msimu baada ya kuumia goti katika mchezo dhidi ya Manchester City (Independent) Jenkinson, 23, anatarajiwa kurejea Arsenal ambao wanafikiria kumuuza Mathieu Debuchy, 30, kwenda Aston Villa (Telegraph). Hayo ni baadhi ya yaliyoandikwa kwenye baadhi ya magazeti ya Ulaya. Zimesalia siku tano kufungwa kwa dirisha la usajili.

SALIM KIKEKE

0 comments:

Chapisha Maoni