Jeshi la Polisi mkoani Iringa limewakamata wahamiaji haramu wanane raia wa Ethiopia waliokuwa wakisafiri isivyohalali na bila kibali cha kuingia nchini wakiwa wamepakiwa kwenye gari ya kusafirisha magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communication.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Peter Kakamba amesema watu hao raia wa Ethiopia wamekamatwa katika kituo cha ukaguzi wa magari Igumbilo manispaa ya Iringa wakati jeshi la polisi mkoani hapa likiwa kwenye operesheni ya kawaida limewakamata raia hao pamoja na mtu mwingine mmoja anayedaiwa kuwa msindikizaji lakini haikufahamika kama alikuwa akisindikiza magazeti ama alikuwa anasindikiza raia hao wa Ethiopia.
Katika tukio lingine kamanda Kakamba amesema mnamo siku ya tarehe 25 gari lenye namba za usajiri T.275 BMW lilikuwa likiendeshwa na Manase Alen mwenye umri wa miaka 29 liligongana na pikipiki iliyokuwa imepakia abiria wawili maarufu mishkaki ambayo haikuweza kufahamika namba zake kutokana na kuharibika vibaya iliyokuwa ikiendeshwa na Filbert Mmale na kuwaua papo hapo dereva huyo wa pikipiki na abiria wawili Emmanuel Kitosi miaka 30 na Hamisi Sigara wote wakazi wa Mseke mkoani Iringa.
0 comments:
Chapisha Maoni