Kabla ya kueleza ni jambo gani linawashangaza watu, kwanza tujifunze kidogo dhana za hisabati.
Kwanza ni mlolongo wa Fibonacci(Fibonacci sequence). Inaanza hivyo: 1, 1, 2, 3, 5, 8, 13, 21, 34, 55, 89, 144...
Katika mlolongo huu, namba inayofuata ni jumla ya namba mbili zinazotangulia.
Tuangalie kwa makini mlolongo huu. Tukigawanya namba moja kwa namba ifuatayo, kwa mfano:
1÷1=1
1÷2=0.5
2÷3=0.666...
3÷5=0.5
5÷8=0.625
……
55÷89=0.617977…
……
144÷233=0.618025…
……
Tutagundua kuwa matokeo yanakaribia zaidi uwiano wa dhahabu(golden ratio). Vitu au sanaa zinazoendana na uwiano huo huwa na sura za kuvutia zaidi.
Tukiangalia maua madogo ya alizeti, tutaona kuna misururu 13 ya mbegu inayokwenda kinyume na mzunguko wa akrabu na misururu 21 inayokwenda na mzunguko wa akrabu. Namba hizi mbili zote ziko kwenye mlolongo wa Fibonacci. Tukiangalia maua makubwa, tutaona namba za 89,144. Misururu ya mbegu ya maua makubwa zaidi hata inaweza kufikia 144 na 233.
Umeshangazwa kwamba kweli kuna miujiza mingi katika maumbile ya kiasili? Kwa nini maua ya alizeti yanaendana na dhana za hisabati? Labda hali hii inayasaidia kubana nafasi na kuzaa mbegu nyingi zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni