Alhamisi, Januari 28, 2016

UN: ULAYA IWAPOKEE WAKIMBIZI ZAIDI

Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa imetoa wito wa kupokewa wakimbizi katika jamii za nchi za Ulaya.
Mkuu mpya wa Kamishena Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa, Filippo Grandi amesema nchi zilizoendelea kiviwanda zina uwezo wa kupokea wakimbizi zaidi licha ya hali tete ya kisiasa inayoshuhudiwa barani Ulaya. Grandi amesema kuwa jamii ya nchi za Ulaya imo katika hali ya kuchakaa na kuzeeka na inahitaji kuchanganyika na wakimbizi kutoka nchi nyingine. Afsia huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, wakimbizi wana mchango mkubwa katika masuala ya jamii. Hata hivyo amesema matukio ya kusikitisha kama mashambulizi ya kigaidi ya Paris yamekuwa na taathira mbaya kwa suala la wakimbizi wanaoelekea katika nchi za Ulaya.
Mkuu wa Kamisheni ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa amezikosoa nchi za Ulaya kwa kufunga au kuweka vizuizi vya mpakani na sheria zisizo za kibinadamu dhidi ya wakimbizi.

0 comments:

Chapisha Maoni