Ijumaa, Januari 29, 2016

CHADEMA KUMSHTAKI NAPE NNAUYE

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitapeleka hoja kwa wananchi juu ya hatua ya serikali ya kusikitisha matangazo ya Bunge moja kwa moja (live) kwenye Televisheni ya Taifa (TBC) kwa madai kuwa ni kulipunguzia gharama shirika hilo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amesema kufuatia  kauli ya Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyotolewa jana bungeni, atapeleka hoja kwa wananchi ili kuona kitendo hicho kama kinakubalika ama la.
Alisema hayo leo katika Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na wanahabari, akisema kutorusha matanagzo hayo ‘live’ ni kumnyima mtanzania haki yake ya msingi kwa kuwa matangazo hayo yanalipiwa na  kodi za wananchi wenyewe.
Alisisitiza kuwa haiwezekani kurushwa baadhi ya vipengele, tena nyakati za usiku, muda ambao televisheni nyingi huonyesha vipindi vya burudani na wananchi wengi pia huwa wamechoka kutokana na kazi.
Aliitaka serikali kutaja kiasi cha fedha zinazotakiwa kurusha matangazo hayo ‘Live’ ili atakapopeleka hoja yake kwa wananchi, wakikubali kuchangia, wajue ni kiasi gani kitatakiwa ili hata kama TBC itakataa, wapeleke kwenye televisheni nyingine.

0 comments:

Chapisha Maoni