Hakuna mtu yeyote anayeweza kusoma namba hii, kwa sababu ina tarakimu milioni 22.33! Ukichapisha namba hizi, urefu wa sentensi utazidi kilomita 65!
Mtaalamu wa hisabati wa Marekani Dr. Curtis Copper alitangaza namba hii Januari mwaka huu. Haina maana yoyote maalum, lakini inawahimiza watu kutengeneza chip nzuri zaidi za kompyuta na kutunga teknolojia nzuri ya kuficha maneno(encryption).
Namba tasa ni nini? Huu ni ujuzi wa shule ya sekondari. Namba tasa inaweza kugawanywa na 1 au yenyewe tu. Uwezekano kwa namba kubwa kuwa tasa ni mdogo sana, hivyo ni vigumu kutafuta namba hizi. Namba mpya iliyogunduliwa na mtaalamu huyu ikiandikwa kuwa namba kipeo (exponential form) si ndefu, yaani 2^74207281-1. Namba hii pia inaitwa namba tasa ya Mersenne. Marin Mersenne ni mtaalamu wa histabati wa karne ya 17, ambayo anatafiti namba tasa inayoweza kuandikwa kwa njia ya 2^p-1. (p ni namba nyingine tasa).
0 comments:
Chapisha Maoni