Jumamosi, Januari 23, 2016

TETESI ZA SOKA ULAYA

Manchester United wamsesimamisha kufanya usajili wowote kutokana na kutokuwepo na uhakika na hatma ya Louis van Gaal (Daily Mirror), wakala wa Alexandre Pato amethibitisha kuwa timu nne ikiwemo Chelsea na Liverpool wana nafasi ya kumsajili mshambuliaji huyo, lakini amesisitiza kuwa hakuna dau lolote lililotolewa (UOL), Tottenham watapewa nafasi ya kwanza kumsajili Gareth Bale, 26, iwapo atauzwa na Real Madrid (Daily Mirror), Shaktar Donetsk wanasema mshambuliaji wao Alex Teixera ana thamani ya pauni milioni 39, wakati Liverpool wakisema wako tayari kutoa pauni milioni 24.5 (BBC Radio 5 live), Zenith St Petersburg wanamtaka meneja wa Manchester City, Manuel Pellegrini kuchukua nafasi ya Andes Villas-Boas mwisho wa msimu (Daily Star), beki wa Chelsea Branislav Ivanovic, 31, anajiandaa kusaini mkataba mpya na kuendelea kulipwa pauni 120,000 kwa wiki (Daily Express), lakini kiungo Nemanja Matic, 27, anafikiria kuondoka Stamford Bridge kutokana na kiwango chake kusuasua (Daily Mail), Manchester United wamemchukua kipa kutoka Poland Bartosz Mrozek, 15, kwa ajili ya majaribio (Przeglad Sportowy), Manchester United wanafikiria kuacha kumfuatilia Filipe Anderson, 22, wa Lazio kutokana na bei kubwa (Bleacher Report), wakala wa Fernando Torres, 31, amesema mshambuliaji huyo atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani hivi karibuni baada ya kupata dau kutoka timu nane. Torres anacheza Atletico Madrid kwa mkopo kutoka AC Milan (Sun), Crystal Palace wanafikiria kumpa Emmanuel Adebayor, 31, mkataba wa miezi sita (Guardian), kiungo wa zamani wa Brazil Ronaldinho, 35, amesema hana mipango ya kustaafu na anatafuta klabu mpya (Goal.com), meneja wa Sunderland amesema anatafuta washambuliaji wawili na kipa, lakini amekataa kuthibitisha kuwa anamtaka Andre Ayew, 26 wa Swansea (Chronicle Live), meneja wa Newcastle amepanda dau la pauni milioni 7 kumtaka mshambuliaji wa Swansea Bafetimbi Gomis, 30 (Sun).

SALIM KIKEKE

0 comments:

Chapisha Maoni