Parachichi ni tunda lenye mbegu moja na virutubisho vingi sana. Hujulikana kama avocado kwa Kingereza, na hulimwa sehemu mbalimbali duniani. Kiasili mapachichi yalianza kulimwa nchini Mexico na Amerika ya Kusini, na baadae kusambaa sehemu zingine duniani ikiwemo Tanzania.
Parachichi limejaa virutubisho vingi, likijulikana kama nutrient dense fruit. Virutubisho vilivyo ndani ya parachichi ni protini, mafuta, vitamini, wanga na madini mbalimbali.
1. Kupunguza Lehemu Mwili
Baadhi ya tafiti zilizofanyika zinaonesha ulaji wa mlo wenye maparachichi kwa wingi kila siku unasaidia kupunguza lehemu mbaya mwilini (LDL cholesterol) na kuongeza lehemu nzuri (HDL cholesterol). Pia matumizi ya parachichi moja kila siku yanasaidia kupunguza lehemu hizi kwa watu wenye uzito mkubwa.
2. Kupunguza Mifupa Kulainika
Vitamini K ni aina ya vitamini ambayo ipo kwa wingi kwenye maparachichi pia. Vitamini hii husaidia unyonywaji wa madini ya Kalsiamu ambayo hujenga mifupa na kuwa imara. Ulaji wa parachichi kila siku au mara kwa mara itakupa madini ya kutosha ya viatmini K ambayo yatasaidia pia unyonywaji wa Kalsiamu. Parachichi moja linakupa kiasi cha asilimia 50 ya mahitaji ya mwili ya Vitamini K kwa siku.
3. Hupunguza Hatari ya Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu.
Kwa kupunguza lehemu mbaya na kuondoa sumu mwilini maparachichi husaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kama shambulio la moyo, angina, shinikizo la damu kupanda na mengine mengi. Pia hupunguza hatari ya magonjwa ya muda mrefu kama kisukari.
0 comments:
Chapisha Maoni