Ijumaa, Januari 15, 2016

PIGO LINGINE KWA WATU WA BURUNDI

Watu sita waliuawa katika maporomoko ya ardhi yaliyosababisha na mvua kubwa iliyokumba jimbo la Makamba kusini mwa Burundi jana (Jumatano),mmafisa walisema.
"Watoto watatu na mama yao waliuawa kwenye maporomoko hayo ya ardhi huko Ndora katika wilaya ya Vugizo walipokuwa wakifanya shughuli za kilimo.Maporomoko mengine ya ardhi yalitokea huko Bukinda katika wilaya ya Nyanza-Lac na kuua mwanamke na mtoto wake."Gavana wa mkoa wa Makamba Gad Niyukuri alisema.
Kulingana na Gavana Gad,mvua hiyo pia ilitoa paa za nyumba 25, na kuacha familia kadhaa bila makazi.

0 comments:

Chapisha Maoni