Ijumaa, Januari 15, 2016

JESHI LA POLISI MKOANI PWANI LIMEFANYA MAAMUZI HAYA MAGUMU

FICHUO inakuletea ripoti kutoka Pwani kama ilivyoandikwa na mwandishi Victor Masangu, taarifa yake imeeleza kuwa ili kukabiliana na wimbi la uharifu Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limepiga marufuku kwa watu wenye tabia ya kukesha katika vilabu vya pombe usiku kucha, na kucheza pool kuanzia asubuhi mpaka usiku wa manene ,hali ambayo ndio imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa vitendo vya wizi, unyang’anyi pamoja na ujambazi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na mikakati waliyojiwekea katika kupambana na uharifu Kamanda wa Polis Mkoa wa Pwani kamishina msaidizi Boniventura Mushongi amesema kwamba kwa sasa wameanza kufanya msako mkali katika maeneo ya Mkoa wa Pwani ya kuwasaka watu ambao wanajihusiha na vitendo vya ujambazi.
Kamanda Mushongi alisema kwamba tabia ya baadhi ya watu kukesha katika maeneo hayo ya vilabu vya pombe wamebaini wanajihusisha na uchezaji wa kamali, uuzaji wa bangi hivyo kupelekea kufanya matukio ya uporaji wa mali za watu katika nyakati hizo za usiku kwa wapiti njia na wale ambao wamekwisha pumzika majumbani kwao
“Jamani waandishi kwa sasa sisi kama jeshi la polisi Mkoa wa Pwani tumejipanga vilivyo na tutafanya msako katika maeneo mbali mbali yote hii ni kuhakikisha wimbi la uharifu linapungua na kwa sasa hatutaki kuona watu wanakesha baa kwani wao ndio chanzo vha kusababbisha kutokea kwa uharifu,”
“Maana kuna baadhi ya watu wanakesha katika vilabu vya pombe kumbe wengine wanavuta muda wa usiku ndipo waanza kufanya matukio yao ya uharifu kwa hiyo hatutakio kuona mtu yoyote anashinda katika vilabu hivyo sambamba na kucheza pool kuanzia asubuhi mpaka saa nane za siku ni marufuku kwanza ni kinyume cha sheria na taratibu ,”alisema Kamanda.
Aidha Kamanda huyo aliwataka wananchi wa Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wazazi kkuachana na uwogo na badala yake sasa wahakikishe wanashirikiana na jeshi la polisi katika kuwafichua wahalifu bila ya kuwa na uwoga wowote na pindi watakapoona wana mashaka na mtu watoe taarifa katika vyombo husika.
Katika hatua nyingine Kamanda huyo alibainisha, sababu nyingine zinazochangia kwa kisi kikubwa kutokea kwa wimbi la uharifu ni kutokana na baadhi ya watu kunywa ombe kupita kiasi pamoja na madereva wa pikipiki kushirikiana na waharifu katika kufanya matukio hayo ya uporaji.
Kufuatia kaluli hiyo iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Tanzania daima iliweza kuzungumza na baadhi ya madereva wa pikipiki akiwemo Hussen Ally pamoja na Nassoro Bala ambao walisema kwamba kuna baadhi ya madereva wa pikipiki wanavunja sheri kwa makusudi ikiwemo kunywa pombe wakati wanaendesha chombo cha moto.
Walisema kwamba wakati mwingine matukio ya uharifu yanajitokeza bila ya wao kujua kwani wakati mwingine wanaweza kupakia abiria zaidi ya mmoja kumbe wote waliopanda ni waharifu na matokeo yake wanapofika njiani wanaipora pikipiki hiyo na kumjeruhi dereva au wakati mwingine wanaamua kumuuwa.
Hata hivyo uchunguzi uliofanyuwa na Mwandishi wa habari hizi uliweza kubaini katika Mkoa wa Pwani kwa sasa bado unakabiliwa na wimbi la uharifu kutokana na baadhi ya vijana wengi wa mitaani kutokuwa na kazi hivyo kujiingiza katika uharifu hali ambayo imekuwa ni tishio sana kwa wananchi hasa katika eneo la maili moja , lililopo Wilaya ya Kibaha, pamoja na eneo la Kiluvya lililopo Wilaya ya Kisarawe hivyo kuhahitajika juhudi za makusudi kwa jeshi la polisi kukabiliana na hali hii.

0 comments:

Chapisha Maoni