Nigeria imeimarisha operesheni ya kutafuta na kukomboa wasichana wa shule ya Chibok waliotekwa usiku wa Aprili 14 mwaka wa 2014 na kundi la kigaidi la Boko Haram, pamoja na watu wengine wanaozuiliwa na kundi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika jimbo la Maiduguri, Isiaka Amao kamanda wa jeshi la anga nchini Nigeria alisema kuwa wanajeshi wake wamefanya mashambulizi 286 ya anga tangu Desemba 25 na kuharibu kambi zinazotumika na kundi hilo. "Mojawapo ya operesheni iliokuwa wa fanaka zaidi ni ile ya Desemba 25 mwaka uliopita ambapo viongozi wakuu wa Boko Haram na makamanda wake wa ngazi za chini waliuawa walipokuwa kwenye mkutano ndani ya msitu wa Sambisa," Amao alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni