Jumapili, Januari 31, 2016

BARCELONA WAZIDI KUCHANJA MBUGA

Mabingwa watetezi wa kombe la Primera Liga, Barcelona jana (Jumamosi) walipiga hatua muhimu ya kutetea taji hilo kwa kuwashinda Atletico Madrid mabao 2-1 katika ukumbi wa Camp Nou.
Ushindi huo sasa umewaweka Barcelona pointi tatu mbele ya wafuasi wao wa karibu Atletico Madrid, na pointi saba mbele ya washindani wao wa jadi Real Madrid ambao kwa sasa wanashikilia nafasi ya tatu. Mabao hayo ya Barca yalifungwa na Leo Messi na Luis Suarez huku upande wa Atletico ukichezewa na wachezaji 9 baada ya Felipe Luis na Diego Godin kupewa kadi nyekundu.

0 comments:

Chapisha Maoni