Jumanne, Januari 26, 2016

MASUALA YALIYOANDIKWA KATIKA KURASA ZA MICHEZO ULAYA

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal, alikuwa tayari kujiuzulu siku ya Jumamosi baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Southampton, lakini akabembelezwa asifanye hivyo na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward (Sun), Van Gaal ambaye amekwenda Uholanzi kwenye sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa kwa binti yake, ataendelea na mazungumzo na Ed Woodward siku ya Jumanne atakaporejea (Guardian), Ed Woodward amezungumza na wachezaji kadhaa, pamoja na maafisa wengine wa ngazi ya juu Old Trafford kuhusu Van Gaal (Sky Sports), hata hivyo Ed Woodward yuko tayari kwenda kinyume na mtazamo wa mashabiki wengi na kuamua kumuacha Van Gaal aendelee kusalia Old Trafford (Mirror), mwandishi wa habari Miguel Delaney amesema Manchester United wanafahamu kuwa Jose Mourinho anataka kumrithi Van Gaal na kuwa mazungumzo kati ya wawakilishi wake na United yamekuwa yakiendelea kwa muda (BBC Radio 5 live), mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 26, ameogopa kuhamia Manchester United kwa pauni milioni 100 kutokana na hali ya mashaka iliyopo sasa kuhusiana na Van Gaal (Independent), winga wa Tottenham Andros Townsend, 24, anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Newcastle, baada ya timu hizo mbili kukubaliana ada ya uhamisho (Guardian), Totteham wana wasiwasi kuwa huenda beki Jan Vertonghen, 28, aliumia zaidi goti lake na huenda asicheze msimu wote uliosalia (Sun), Newcastle watapanda dau jingine kutaka kumsajili Alexandre Lacazette, 24, kutoka Lyon, baada ya mchezaji huyo kusema hataki kwenda Newcastle (Telegraph), Liverpool wamegonga mwamba katika dau lao la pauni milioni 28 kutaka kumsajili mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk, Alex Teixeira, ambaye amepachika mabao 22 katika mechi 15 msimu huu (Mail), West Brom wanataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli, 25, anayechezea AC Milan kwa mkopo (Express & Star), matumaini ya Newcastle kumsajili Loic Remy, 28, kutoka Chelsea yatategemea na kukamilika kwa usajili wa Alexandre Pato kutoka Corinthians kwenda darajani (Chronicle), Sunderland kwa mara nyingine tena wamehusishwa na mshamuliaji kutoka Ivory Coast, Seydou Doumbia, 28, anayecheza Roma na ambaye inadaiwa amekataa mkataba wa fedha nyingi kwenda China (Sunderland Echo), West Ham wamekubaliana na mshambuliaji kutoka Nigeria Emmanuel Emenike, 28, lakini bado hawajaafikiana na klabu yake Fernabahce, na Al Ain ya Imarati anapocheza kwa mkopo (Evening Standard), Watford wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Fiorentina Mario Suarez, 28 (Watford Observer). Hayo ni baadhi ya yaliyoandikwa kwenye baadhi ya magazeti ya Ulaya. Zimealia siku sita kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

SALIM KIKEKE

0 comments:

Chapisha Maoni