Gazeti la Times la nchini Uingereza limefichua kuwa, filamu ya matukio ya kweli itatengenezwa hivi karibu kuhusu tabia ya ulevi, uasherati na uchezaji kamari aliyokuwa nayo Mfalme wa zamani wa Saudia, Fahd bin Abdulaziz.
Shirika la Habari la IRIB limelinukuu gazeti hilo la nchini Uingereza likisema kuwa, filamu hiyo yenye anuani ya "Udhaifu wa Mfalme Fahd" itafichua siri za maisha ya machafu ya mtawala huyo wa zamani wa Saudia. Filamu hiyo itatengenezwa kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na Bi. Janan Harb, mke wa zamani wa Fahd bin Abdulaziz mfalme wa zamani wa Saudia ambaye alitimuliwa nchini humo na sasa anaishi nchini Uingereza. Mjane huyo wa Fahd bin Abdulaziz ameamua kubadilisha kisa chake cha kweli kuwa filamu. Katika filamu hiyo anafichua namna mfalme Fahd alivyokuwa mcheza kamari na mraibu wa vidonge vya kutuliza mauamivu.
Bi. Harb anasema mfalme wa sasa wa Saudia, Salman bin Abdulaziz, wakati akiwa gavana wa Riyadh ndiye aliyeshinikza apewe talaka na Fahd na kisha kutimuliwa Saudia. Anamtaja Mfalme Salman kuwa, 'Katili wa Riyadh' kwani katika zama zake za ugavana aliwanyoga watu wengi sana mjini humo. Gazeti la Times la Uingereza limeandika kuwa filamu hiyo inatengenezwa wakati ambapo Saudia inakabiliwa na matatizo chungu nzima kutokana na kuporomoka bei ya mafuta duniani. Gazeti hilo limeandika kuwa hivi sasa watawala wa Saudia wanajaribu kuficha habari zilizoenea kuhusu kuwepo mizozo ya kugombania madaraka ndani ya ukoo unaotawala wa Aal Saud.
Gazeti hilo limedokeza kuwa, kuna video zinazomuonyesha Fahd bin Abdulaziz akiwa katika klabu ya kamari ya Claremont ya London huku akiwa amelewa chakari huku akitumia tembe za mihadarati aina ya methadone na akicheza kamari.
Gazeti hilo limeandika kuwa tabia hiyo ya chafu aliyokuwa nayo mfalme huyo na ambayo imelaaniwa na watu wengi kwani wafalme wa Saudia kwa kawaida kujipachika anwani ya 'Khadimul Haramein' yaani mhudumu wa misikiti miwili mitakatifu. Alipohojiwa na gazeti hilo , mjane huyo wa Fahd bin Abdulaziz amesema kuwa, mwaka 1968 akiwa na umri wa miaka 20 aliolewa na Fahd ambaye wakati huo alikuwa mritihi wa kiti cha ufalme na waziri wa mambo ya ndani wa Saudia. Amesema kuwa, wazazi wake ambao ni Wapalestina walikuwa wakiishi Riyadh wakati huo na aliweza kumvutia kirahisi Fahd kutokana na kuvaa kwake nguo fupi zinazoonesha maungo ya mwili wake.
0 comments:
Chapisha Maoni