Jumanne, Januari 26, 2016

DALILI 5 ZA KIHARUSI

Kiharusi hutokana na seli za ubongo kushindwa kufanya kazi pale zinapokosa damu kutokana na mishipa ya damu ya ubongo kuziba au kupasuka. Mara nyingi kiharusi hutokea ghafla, lakini kuna dalili unazoweza kupata kuashiria ugonjwa huu.
Dalili hizi zinaweza kuwa zifuatazo:
1. Kukosa nguvu au kupata ganzi kwenye uso, mkono au mguu, hasa upande mmoja wa mwili.
2. Hali ya kuchanganyikiwa au kushindwa kuongea ghafla.
3. Kushindwa kuona vizuri ghafla.
4. Kushindwa kutembea au kupata kizunguzungu kikali kwa ghafla.
5. Maumivu makali ya kichwa ghafla.
Kiharusi ni ugonjwa unaohitaji matibabu haraka sana. kadri mgonjwa anapozidi kuchelewa kupata mtibabu ndivyo seli za ubongo zinavyozidi kufa. Kufa kwa seli hizi kutasababisha ulemavu kwa mgonjwa.

0 comments:

Chapisha Maoni